Kenya yabuni uhusiano wa kidiplomasia na Visiwa vya Solomon

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na mwenzake wa Mambo ya Nje na biashara ya Kimataifa wa Visiwa vya Solomo, walitia saini mkataba wa kubuniwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Visiwa vya Solomon Rick Nelson Houenipwela.

Kenya inaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia kote duniani, hatua ya hivi punde ikiwa kubuni uhusiano wake na Visiwa vya Solomon.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na mwenzake wa Mambo ya Nje na biashara ya Kimataifa wa Visiwa vya Solomo, walitia saini mkataba wa kubuniwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye mkutano huo ulioandaliwa  pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani, Mudavadi alisema hatua hiyo inafungua ukurasa mpya kwa Kenya katika eneo la Pacific, na kubuni msingi wa ushirikiano katika biashara, uchumi wa majini, kukabiliana na tabianchi na ubadilishanaji wa ujuzi.

Wakati huo huo, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alisema ushirkiano huo wa kidiplomasia na Visiwa vya Solomon, pia utawezesha mataifa hayo mawili kukabiliana na maswala ya kimataifa, yanayowaathiri raia wa mataifa hayo.

“Kwa raia wa Kenya, hususan vijana wetu na wafanyabiashara, uhusiano mpya wa kimataifa una uwezo wa kufungua masoko mapya, ushirikiano na fursa mbali mbali,” alisema Mudavadi.

Share This Article