Mwanamuziki wa Uganda Carol Nantongo amesema uzazi umebadilisha kabisa maisha yake, akifichua kwamba kwa sasa yeye hutumia muda mwingi na mtoto wake mchanga huku akiendelea kujitolea katika kazi yake ya muziki.
Nantongo amefunguka kuhusu jinsi uzazi ulivyobadilisha mtindo wake wa maisha, akisema kuwa sasa hutumia muda mwingi nyumbani akimtunza mtoto wake mchanga.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda, Nantongo alisema kuwa mama kumebadilisha kabisa ratiba yake ya kila siku pamoja na vipaumbele vyake.
Alieleza kuwa kabla ya kujifungua, mara nyingi alikuwa akitumia jioni zake kufurahia maisha ya usiku jijini Kampala. Hata hivyo, siku hizo sasa zimepita kwani anatumia muda wake mwingi kumlea mtoto wake.
“Uzazi umenibadilisha sana. Maisha sasa ni tofauti kabisa. Mimi htumia muda wangu mwingi nikiwa nyumbani na mtoto wangu.” Alielezea mrembo huyo.
Aliendelea kusema kwamba hata simu yake huwa haigusi sana kama awali na huwa haendi tena matembezini kama alivyokuwa akifanya zamani kwa sababu mtoto wake anamhitaji.
Licha ya mabadiliko yanayoambatana na kuwa mama, Nantongo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuachana na muziki. Alisema anaendelea kujitolea katika kazi yake ya muziki huku akiyakumbatia majukumu yake mapya kama mama.
Kama ilivyo kwa wasanii wengine wa kike kutoka Uganda, akiwemo Cindy Sanyu, Sheebah Karungi, na Vinka, Nantongo anatarajia kusawazisha majukumu ya uzazi na kujenga taaluma yenye mafanikio katika muziki.