Mwanamke apatikana ameuawa Kitui

KBC Digital News
1 Min Read

Mwanamke mmoja anayeaminika kuwa mwenye umri wa kati ya miaka 30 na 35 amepatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika kijiji cha Savani mjini Kitui.

Mwili huo uliripotiwa kuanza kuoza na ulikuwa na majeraha, ikiashiria marehemu huenda alinyanyaswa kingono na kuchomwa kisu machoni.

Kisa hicho kimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kitui ya Kati Peter Karanja.

Karanja amesema hakuna ripoti yoyote iliyopigwa juu ya  kutoweka mtu yeyote kuhusiana na kisa hicho.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitui kuhifadhiwa wakati uchunguzi ukiendelea.

Taarifa ya KNA

Share This Article