Jeshi la Uganda lakamilisha maandalizi ya uapisho wa Museveni

Dismas Otuke
1 Min Read

Jeshi la Uganda limekamilisha maandalizi ya sherehe ya kumuapisha Rais Yoweri Kaguta Museveni, kwa muhula wa saba Mei 12, katika uwanja wa Kololo jijini Kampala.

Aidha, jeshi hilo limesema kuwa litadhibiti idadi ya watu watakaoingia katika uwanja wa Kololo.

Marais kadhaa ,Mabalozi na wageni mashuhuri pia wanatarajiwa katika uapisho huo.

Pia watakaoingia uwanja huo watafanyiwa ukaguzi huku baadhi ya barabara za kutoka na kuingia jijini zikitarajiwa kufungwa.

Wageni wapatao 40,000, wanatarajiwa kuudhuria hafla hiyo ambayo pia italandana na maadhimisho ya miaka 40 uongozini kwa Rais Museveni.

Serikali pia imetangaza Mei 12 kuwa siku  ya mapumziko.

Museveni aliye na umri wa miaka 81, alishinda muhula wa saba katika uchaguzi mkuu wa Januari mwaka huu, akipata takriban asilimia 72 ya kura zote.

 

Share This Article