Mshambulizi wa klabu ya Nairobi United maarufu kama Naibos, Kevin Wangaya, ndiye mchezaji bora katika Ligi kuu ya Kenya mwezi wa Aprili.
Mwanandinga huyo aliye anayeichezea timu ya Kenya kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, amefuata nyayo za chipukizi wa Kariobangi Sharks, Humphrey Aroko, aliyenyakua tuzo hiyo Februari mwaka huu.
Wangaya amechezea timu zote za taifa kwa chipukizi na sasa ndoto yake ni kuichezea Harambee Stars, katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka ujao.
Katika mwezi Aprili,Wanganya alifunga mabao matatu na kuchangia mengine matatu katika mechi tano alizowakilisha Nairobi United, wakikosa kushindwa mwezi jana.
Waganya amepokea tuzo na shilingi 50,000 kwa ushindi wake.