NTSA kurejesha Alcoblow eneo la Pwani mwezi Agosti kuzuia ajali barabarani

Aidha, NTSA imewataka raia kupiga ripoti ya visa vya madereva wanaoendesha magari wakiwa wamebugia mtindi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya Kitaifa Uchukuzi na Usalama (NTSA) imetangaza kurejesha matumizi ya vifaa vya Alcoblow katika ukanda wa Pwani kuanzia mwezi ujao wa Agosti ili kuzuia ajali za barabarani.

Katika taarifa kwa wanahabari, afisi ya NTSA kaunti ya Mombasa, kwa ushirikiano na Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS ) imesema matumizi ya alcoblow yatapunguza ajali zinazosababishwa na madereva walevi.

Aidha, NTSA imewataka raia kupiga ripoti ya visa vya madereva wanaoendesha magari wakiwa wamebugia mtindi.

Kumekuwa na visa vya mara kwa mara vya ajali barabarani ambavyo vimeripotiwa katika siku za hivi karibuni, huku vingi vya visa hivyo vikiripotiwa kusababishwa na sababu za kibinadamu.

Sababu hizo zinajumuisha ulevi na utepetevu kwa upande wa madereva.

Raia wamekuwa wakitoa wito kwa mamlaka kuingia kati ili kuepusha maafa yanayoweza yakaepukika barabarani.

Share This Article