Jacob Oboth ndiye Spika mpya wa bunge nchini Uganda

Oboth aliye na umri wa miaka 55, amerithi kiti hicho kutoka kwa Anita Among

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunge la Uganda limemchagua Jacob Oboth kuwa Spika wa bunge la 12, baada ya kuandaa uchaguzi.

Oboth ambaye pia ni Mbunge wa West Budama County South, kwa tiketi ya chama cha NRM, ametangazwa mshindi baada ya kuzoa kura 441, katika uchaguzi wa mapema Jumatatu.

Mbunge wa Jinja Paul Mwiru wa chama cha National Unity Platform (NUP), amemaliza wa pili kwa kura 60.

Oboth aliye na umri wa miaka 55, amerithi kiti hicho kutoka kwa Anita Among ,anayezongwa na masaibu chungu nzima kuhusiana na kashfa za ufisadi.

Uchaguzi huo umeandaliwa katika uwanja wa kihistoria wa Kololo, na kuhushudiwa na Rais Yoweri Museveni.

Share This Article