Magari mawili ya kifahari yanaswa nyumbani kwa Spika wa Uganda

Haya yanajiri huku serikali ikiendesha msako mkali dhidi ya Among kuhusiana na madaia ya ufisadi na ufujaji pesa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Idara ya Upelelezi jijini Kampala nchini Uganda siku ya Jumatano walinasa magari mawili ya kifahari kutoka nyumbani kwa Spika wa bunge la kitaifa anayeondoka Anita Among.

Gari la tatu lililopatikana na kubebwa kutoka eneo la Nakasero nyumbani kwa Among, lilikuwa aina ya Mercedes-Maybach, huku la nne likiwa aina ya Lexus -UBP 704Y.

Magari hayo yanaongezea kwa yale ya Roll Ryce na Range Rover, yaliyokamatwa na kubebwa wiki jana.

Haya yanajiri huku serikali ikiendesha msako mkali dhidi ya Among kuhusiana na madai ya ufisadi na ufujaji pesa.

Masaibu na shinikizo hizo zimemlazimu Among, ambaye ni mumewe Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Uganda Moses Magogo, kujiondoa kutetea kiti cha Spika.

Share This Article