Alamisi,Chepkirui na Lemiso kushiriki majaribio ya dunia chipukizi

Alamisi,Chepkirui na Lemiso kushiriki majaribio ya dunia chipukizi

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mtetezi wa Dunia katika mbio za mita 5000 Andrew Kiptoo Alamisi ,bingwa wa Afrika wa mita 3000, kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 Cynthia Chepkirui, ni miongoni mwa wanariadha watakaoshiriki majaribio ya kitaifa kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, baina ya Alhamisi na Jumamosi, hii katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Kiptoo aliyeshinda dhahabu ya Dunia mwaka 2024, mjini Lima Peru, atawania tiketi ya kutetea taji yake ya mita 5,000, pamoja na wanariadha wengine 18, wanaowania nafasi mbili za kufuzu.

Chepkirui aliye na umri wa miaka 17 na aliyeshinda dhahabu ya Afrika, mwaka jana nchini Nigeria, atakabiliana na mshindi wa nishani ya shaba ya Afrika katika mita 3000, kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, Joyline Chepkemoi, na Sheila Chepng’eno, miongoni mwa wengine.

Bingwa wa Afrika kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18, katika mita 2000 kuruka viunzi na maji Emmanuel Lemiso, atatimka mita 3000, kuruka viunzi na maji pamoja na Felix Kiptoo na Evans Kipkemboi miongoni mwa wengine.

Chama cha Riadha Kenya, kinatarajiwa kuwateua wanariadha wapatao 30 kwa mashindano ya Dunia, yatakayoandaliwa Mjini Eugine Marekani, baina ya Agosti 5 na 9 mwaka huu.

Share This Article