Kindiki atetea mipango ya serikali ya kudhibiti bei ya mafuta

Ameahidi kuwa serikali imejitolea kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta ili kuzuia kupanda kwa gharama ya maisha.

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki ametetea mipango iliyowekwa na serikali ya kudhibiti kupanda kwa bei ya mafuta nchini Kenya.

Prof. Kindiki amesema kuwa ni lazima kwa serikali kuainisha kati ya kuwakinga wananchi dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta na kuhakikisha huduma za serikali hazikwami.

Akizungumza siku ya Jumatano wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Miseleni-Mwala eneo bunge la Mwalai, kaunti ya Machakos, Kindiki alikiri kuwa serikali inaelewa mzigo wa wananchi kutokana na kuongezwa kwa bei ya mafuta.

Aliahidi kuwa serikali imejitolea kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta ili kuzuia kupanda kwa gharama ya maisha.

Kindiki alifafanua kuwa serikali tayari imetoa shilingi bilioni 13 katika mpango wa kudhibiti bei ya mafuta nchini.

Share This Article