Kipchoge awasili Cape Town, kushiriki Sanlam Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mbio za marathon,Eliud Kipchoge, alitua mjini Cape town Afrika,Kusini, kushiriki mbio za Sanlam Marathon, Jumamosi na Jumapili hii.

Kipchoge atakuwa akishiriki mbio za marathon barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Mwanariadha huyo ambaye ni mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Dunia, ametangaza kushiriki mbio saba za Marathon katika mabara yote saba.

Lengo la kukimbia mbio hizo ni  kuonyesha uwezo wa mwanadamu usiokuwa na vipimo.

Mbio za Sanlam zinalenga kujumuishwa katika msururu wa mbio kuu za marathon ulimweguni.

Share This Article