Tanzania kukabana koo na Afrika Kusini siku ya pili WAFCON

Katika makala ya mwaka 2024, Tanzania walipoteza mechi mbili lakini wakafanikiwa  kupata sare dhidi ya mabingwa wa mwaka huo ambao pia ni wapinzani wa leo, Afrika Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Twiga Stars ya Tanzania watashuka uwanjani Al Medina Jumatatu usiku kwa mechi ya ufunguzi ya kundi B dhidi ya mabaingwa wa mwaka 2022 Afrika Kusini kuanzia saa mbili usiku.

Tanzania watakabiliana na Banyana Banyana wakati kila mmoja akilenga kuanza vyema ili kujiweka katika nafasi bora  ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Twiga Stars wanashiriki michuano ya WAFCON kwa mara ya tatu baada ya kucheza makala ya mwaka 2010 na 2024, ingawa walibanduliwa katika hatua ya makundi.

Katika makala ya mwaka 2024, Tanzania walipoteza mechi mbili lakini wakafanikiwa  kupata sare dhidi ya mabingwa wa mwaka huo ambao pia ni wapinzani wa leo, Afrika Kusini.

Banyana Banyana watakuwa wakishiriki kipute cha mwaka huu kwa mara ya 14, wakijivunia kuibuka mabingwa mwaka 2022.

Baadaye, saa tano usiku,  Burkina Faso watapimana ubabe na Ivory Coast ikiwa derby ya Afrika magharibi katika mchuano mwingine wa kundi B.

Burkinabe wanashiriki WAFCON kwa mara ya pili baada ya mwaka 2022, walipobanduliwa katika hatua ya makundi.

Ivory Coast nao wanacheza WAFCON kwa mara ya tatu baada ya kucheza mwaka 2012 na 2014, huku wakijivunia kumaliza nafasi ya tatu mwaka 2014.

 

 

Share This Article