Kenya yashindwa robo fainali na Afrika Kusini huko Hong Kong

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya timu ya taifa ya raga ya Kenya kucheza nusu fainali ya Kombe kuu kwenye mashindano ya dunia ya wachezaji saba mkondo wa Hong Kong, imeyeyuka baada ya kushindwa na Afrika Kusini alama 26-22 Jumamosi Adhuhuri.

Kenya walianza vibaya mechi hiyo ya robo fainali wakiwa chini alama 12-14, kufikia mapumziko,John Okeyo  na Denis Abukuse wakifunga tries,wakati Blitzbok wakifunga kupitia kwa Selvyn Davids  na Donavan Don.

Shujaa walijizatiti kipindi cha pili kwa matao ya juu Kevin Wekesa na Festus Shiasi wakiongeza try moja kila mmoja ila Afrika Kusini wakajibu kupitia kwa Quewin Nortje  na  Siviwe Soyizwapi.

Afrika Kusini waliizidia Kenya maarifa baada ya kuunganisha conversions 3, huku Kenya wakiunganisha moja pekee.

Shujaa walijikatia tiketi kwa robo fainali baada ya kuwashinda Marekani pointi 17-10, katika pambano la mwisho la kundi C.

 

Share This Article