Gor Mahia watamba huku Posta na Murang’a Seal wakitoshana

Dismas Otuke
1 Min Read

Waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, wamesajili ushindi wa nne kwa mpigo baada ya kuwapiga Mathare United mabao 2-0, katika moja ya mechi mbili za Ligi zilizochezwa leo.

Shariff Musa na Bryson Wangai walipachika bao moja kila mmoja katika mchuano uliosakatwa uwanjani Kasarani.

Ushindi huo umewachupisha K’ogalo hadi nafasi ya pili kwa alama 12, moja nyuma ya viongozi Kakamega Homeboyz.

Posta Rangers wamepoteza uongozi na kulazimishwa kutoka sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Murang’a Seal.

 

 

Website |  + posts
Share This Article