Mabingwa wa Uganda, Vipers waing’ata Gor Mahia na kufuzu nusu fainali

Ushindi huo umeifanya Vipers kuwa timu ya kwanza kujikatia tiketi kwa nusu fainali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Kenya,Gor Mahia FC wameambulia kichapo cha bao moja kwa bila kutoka mabingwa wa Uganda,Vipers SC katika mchuano wa pili wa kundi A,kuwania Kombe la CCEAFA,Kagame uliopigwa Jumatatu alasiri katika uwanja wa Pele mjini Kigali, Rwanda.

Timu zote zilitoka sare tasa katika kipindi cha kwanza na mechi ikielekea ukingoni Gusto Mulongo aliwaduwaza Gor katika dakika ya 93, na kuwapa ushindi maridhawa.

Ushindi huo umeifanya Vipers kuwa timu ya kwanza kujikatia tiketi kwa nusu fainali.

Gor walikuwa wamefungua mashindano kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya wenye APR ya Rwanda, huku mabingwa wa Uganda,Vipers wakiipiga FC Garde Republicane  ya Djibouti mabao 2-0.

K’ogalo sasa wana shinikizo la kuwashinda FC Garde Republicane ili kufuzu kwa nusu fainali.

Share This Article