Mshukiwa wa uhalifu akamatwa Nairobi

Kwenye operesheni yake ya hivi punde katika eneo la Laini Saba, Kibra, jijini Nairobi,  polisi wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la wezi lijulikanalo kama Panga Squad.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa uhalifu akamatwa Nairobi.

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS imesema imeimarisha vita dhidi ya uhalifu kote nchini huku ikitekeleza operesheni zinazolenga kuangamiza makundi ya wahalifu.

Kwenye operesheni yake ya hivi punde katika eneo la Laini Saba, Kibra, jijini Nairobi,  huduma hiyo imedokeza kuwa imemkamata mshukiwa anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la wezi lijulikanalo kama Panga Squad.

Kupitia ukurasa wa X, NPS ilisema iliwafumania watu walioshukiwa kuwa wahalifu lakini walitoroka na kusababisha maafisa hao kuwaandama, hatua iliyofanikisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo akiwa amejihami kwa panga.

Aidha, kulingana na polisi, uchunguzi wa mapema umebaini kwamba mshukiwa huyo ni kiongozi wa genge hilo linalohusishwa na wizi wa kimabavu, na kuwahangaisha wakazi wa mtaa wa Kibra.

Mshukiwa huyo anauzuiliwa kwenye korokoro  ya polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.

NPS imesema operesheni za kuwakamata wahalifu kote nchini zitaendelea na kuwataka raia kutoa habari kwa polisi kuhusu watu wanaowashuku.

Share This Article