Watu 27 wajeruhiwa kwenye ajali barabara ya Nairobi-Mombasa

Shirika la Msalaba mwekundi nchini Kenya, lilisema  ajali hiyo ilihusisha basi, trela, magari mawili ya kibinafsi na pikipiki moja.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu27 wajeruhiwa kwenye ajali katika eneo la Salama kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa.

Watu 27 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Salama, kwenye barabara ya Mombasa-Nairobi Jumapili usiku.

Likithibitisha ajali hiyo, Shirika la Msalaba Mwekundi nchini Kenya, KRC lilisema  ajali hiyo ilihusisha basi, trela, magari mawili ya kibinafsi na pikipiki moja.

Kupitia ukurasa wa X, KRC ilidokeza kuwa maafisa wake walishirikiana na maafisa wa polisi na wale wa kaunti kutoa huduma katika sehemu ya tukio usiku kucha na kukamilisha shughuli hiyo Jumatatu alfajiri.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Sultan Hamud kwa matibabu, huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Share This Article