Vlabu vya Migori Youth, 3K FC na Mombasa United vimefanikiwa kupandishwa ngazi kushiriki katika Ligi Kuu ya Kenya msimu ujao kufuatia kukamilika kwa msimu wa mwaka 2025/2026 wa Ligi ya FKF NSL siku ya Jumapili.
Migori Youth ilifuzu baada ya kutwaa ubingwa wa NSL kwa kuzoa jumla ya alama 80.5 zaidi ya 3K iliyo ya pili huku Mombasa United ikishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 74.
Kando na kupandishwa ngazi, Migori Youth walitawazwa mabingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-1 siku ya Jumapili dhidi ya Equity Bank.
Timu hizo tatu zitatwaa nafasi za Kariobangi Sharks, Bidco United na Sofapaka zilizoshushwa daraja kutoka ligi kuu ya FKF msimu uliokamilika.