Marais Tshisekediki,Kiir na Mahamud, wawasili Uganda kwa uapisho wa Museveni

Aidha, Museveni amefanya mazungumzo na wageni wake katika Ikulu ya Entebe sawia na kikao kingine cha faragha na Afisa mkuu na mwakilishi wa Rais wa Marekani Donald Trump, Nick Checker.

Dismas Otuke
1 Min Read

Marais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud,Taye Atske Selassi wa Ethiopia, na Salva Kiir wa Sudan Kusini wamewasili Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais Yoweri Museveni .

Aidha, Museveni amefanya mazungumzo na wageni wake katika Ikulu ya Entebe, sawia na kikao kingine cha faragha na Afisa mkuu na mwakilishi wa Rais wa Marekani Donald Trump, Nick Checker.

Uapisho wa Museveni utaandaliwa katika uwanja wa Uhuru wa Kololo viungani mwa jijini kuu Kampala, huku viongozi na waakilishi kutoka mataifa 35 ya Afrika na washirika wengine wa karibu wa Uganda, wakitarajiwa kuhudhuria.

Kaguta Museveni aliye na umri wa miaka 81,lichaguliwa kwa muhula wa saba afisini baada ya kuzoa asilimia 71.65 ,ya kura katika uchaguzi Mkuu wa Januari mwaka huu.

Serikali imetangaza Jumanne Mei 12, kuwa siku ya mapumziko ili kuwaruhusu wananchi wengi kuhudhuria sherehe hizo.

Wageni  zaidi ya 30,000 wanattarajiwa kuhudhuria hafla ya uapisho wa Museveni.

 

Share This Article