Rais William Ruto siku ya Jumatatu ameshuhudia ufunguzi wa upanuzi wa afisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi.
Umoja wa mataifa umeekeza dola bilioni 1.1 za Kimarekani, kwa ukarabati na uboreshaji wa miundombinu itkayoungisha afisi hizo za Girigiri, kama vile barabara,uwekaji taa za barabarani,usafishaji wa mto Nairobi,kuweka mitambo ya teknolojia ya kiusalama na kufungua duka la kisasa la Umoja wa Mataifa.
Ruto ametaja uekezaji katika upanuzi wa afisi hiyo kuwa dhidhirisho la mchango mahususi wa Nairobi, kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika na Kusini mwa ulimwengu.
Aliongeza kuwa uboreshaji wa Ukumbi wa Bomas kutaiwela Kenya katika nafasi nzuri ya kuandaa mikutano ya kimataifa.

Ruto aliweka jiwe la msingi kwa upanuzi wa afisi za Umoja wa Mataifa eneo la Gigiri,.
Halfla hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.