Trump akataa ofa ya Iran ya kumaliza mapigano

Trump anatarajiwa kumsukuma Rais wa Uchina Xi Jinping, ambao ndio mnunuzi mkuu wa mafuta ya Iran, atakapozuru Beijing Alhamisi wiki hii.

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Marekani Donald Trump, amakatalia mbali mapendekezo ya Iran, kumaliza mapigano katika eneo la mashariki ya kati na kuongeza uwezekano wa bei ya mafuta kupanda zaidi.

Iran iliijibu Marekani Jumapili kuwa haitasita kujibu mashambaulizi endapo Marekani, itaishambulia ama kuruhusu meli zaidi kuingia katika mlango wa bahari wa Strait of Hormuz.

Hatua ya Trump kukataa ofa ya majadiliano iliyotolewa na Iran, imezua hofu zaidi kuhusu uwezekano wa hali kuwa tete zaidi katika Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, alichapisha kwenye mtandao wake wa X Jumapili kuwa ‘kujitolea kufanya majadiliano hakumaaninishi kuogopa wala kujiondoa kwenye vita’.

Trump anatarajiwa kumsukuma Rais wa Uchina Xi Jinping, ambao ni wanunuzi wakuu wa mafuta ya Iran, atakapozuru Beijing Alhamisi wiki hii.

TAGGED:
Share This Article