Jamaa ajitoa uhai Tanzania baada ya kupokonywa mpenzi

Marion Bosire
2 Min Read

Venance Haule wa umri wa miaka 24 mkazi wa eneo la Idundilanga mji wa Njombe amejitoa uhai kwa kutumia pazia ndani ya chumba chake kutokana na msongo wa mawazo na hasira baada ya kupokonywa mpenzi wake.

Mpenzi wake anasemekana kuchukuliwa na wazazi wake.

Kisa hicho kilithibitishwa na kamanda wa Polisi mkoani Njombe Mahamoud Banga akielezea kwamba mwanaume huyo aliamua kujitoa uhai kwa sababu ya kusumbuliwa na wakwe zake.

Wazazi wa msichana huyo kwa jina Rose Josephat wamekuwa wakimdhalilisha Haule wakitaka amtolee mahari huku wakimtishia kwamba alioa mwanafunzi.

Rose aliacha shule mwaka 2022 akiwa katika kidato cha pili katika shule ya upili ya Kichiwa.

Kulingana na Banga, Haule hajakuwa na amani kwa muda mrefu ambapo amekuwa akishambuliwa na watu waliokuwa wakijisingizia kuwa maafisa wa polisi wakitaka kumkamata kwa kuoa mwanafunzi.

Lengo kuu la vitendo vya kila mara vya watu hao lilikuwa kupata hela kutoka kwake kama hongo ya kuzuia asikamatwe.

Tukio la mwisho lilikuwa la familia ya Rose kufika kwenye makazi yao na kutaka mahari la sivyo wamchukue.

Haule ambaye alikuwa anajihusisha na shughuli za ujenzi hakuweza kutoa mahari na hivyo mkewe akatwaliwa.

Kwenye ujumbe aloacha kabla ya kujitoa uhai, Haule alisema anampenda sana Rose na akamsihi amtunze vizuri mwanao atakayezaliwa.

Share This Article