Maafisa wa afya wamemuweka mtu mmoja karantini katika Hospitali ya Mafunzo na Matibabu Maalum ya Moi, jijini Eldoret, kufuatia uwezekano alitangamana na mtu aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Maafisa wa Wizara ya Afya, wameimarisa juhudi za kuwafuatilia waliotangamana na waathiriwa wa Ebola, kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Kupitia kwa taarifa, Afisa Mkuu wa hospitali hiyo Dkt Philip Kirwa, alisema mtu huyo alitambuliwa kupitia ufuatiliaji wa watu waliokuwa wametangamana na waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Hata hivyo, Kirwa alifafanua kuwa, hospitali hiyo haina wagonjwa walioambukizwa Ebola, huku akionya dhidi ya kuchanganya hatua za karantini na maambukizi yaliyothibitishwa.
Kulingana na Kirwa, mtu huyo atasalia chini ya uangalizi kwa siku 21 na ataruhusiwa kuondoka ikiwa hataonyesha dalili za ugonjwa huo katika kipindi hicho.
Kenya imenakili visa tisa vya ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo, huku mtu mmoja akifariki kutokana namakali ya ugonjwa huo tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha ugonjwa huo nchini Kenya, Oktoba 6, 2026.