Kenya inatarajiwa kupokea chanjo mpya ya ugonjwa wa Mpox, iliyozinduliwa Agosti 27 mwaka huu.
Chanjo hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa nchini baadaye mwezi huu, itawezesha utoaji wake haraka kwa wagonjwa na wakati wa dharura.
Mpango huo unafadhiliwa na shirika la Gavi, The Vaccine Alliance pia unajumuisha Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Madaktari wasio na Mipaka na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus alitaja uzinduzi huo kuwa hatua kubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa Mpox.
Haya yanajiri wakati Kenya ikiripoti vifo vingi kutokana na Mpox miongoni mwa mataifa ya Afrika kati ya mwezi Februari na Machi, ambapo watu wanne walifariki kati ya vifo vyote 78 vilivyoripotiwa barani Afrika.