Owalo kugombea urais kwa chama cha PPP 2027

Martin Mwanje
1 Min Read
Eliud Owalo akitangaza nia yake ya kugombea urais kwa chama cha PPP

Waziri wa zamani wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Eliud Owalo ametangaza kuwa atagombea wadhifa wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kwa chama kipya cha People’s Prosperity Party (PPP). 

Mapema mwaka huu, Owalo alijiuzulu wadhifa wake kama Naibu Mkuu wa Wafanyakazi katika Ofisi ya Rais na kutangaza kuwa atagombea urais mwakani.

“Leo, natangaza rasmi kuwa nadhamiria kugombea urais wa Kenya kwa ticket ya chama cha People’s Prosperity Party,” alisema Owalo wakati akiwahutubia wahanahari leo Jumatano.

“Nitatoa uongozi mzuri na kuzingatia utawala wa sheria. Mwezi Agosti mwaka ujao, tutaanza ukombozi wa tatu wa nchi hii.”

 

Share This Article