Nahodha wa Argentina Lionel Messi angali kushikili kukutu chati ya ufungaji mabao katika makala ya 23 ya kipute cha Kombe la Dunia kinachoendelea katika mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.
Baada ya siku 27 za mashindano, jumla ya mechi 96 zimechezwa na magoli 280 kufungwa ikiwa ni wastani wa mabao 2.9 kwa kila mechi.
Idadi jumla ya mashabiki waliohudhuria mechi hizo katika viwanja 16 vilivyokuwa katika miji 16 tofauti ni milioni 6.25, ikiwa wastani wa mashabiki 65,204 katika kila mchuano.
Messi anaongoza ufungaji mabao kwa magoli 8, moja zaidi ya Kylian Mbappe wa Ufaransa na Erling Halaand wa Norway, wakati nahodha wa Uingereza Harry Kane akipachika mabao 6.
Leo Jumatano ni siku ya mampumziko kabla mechi za robo fainali kuanza Alhamisi Julai 9.
Wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia mashindanoni Morocco watakabiliana na Ufaransa saa tano usiku.
Ijumaa, Uhispania itachuana na Ubelgiji nao Uingereza itaweka miadi na Norway Jumamosi usiku kabla ya Argentina kumaliza udhia na Uswizi mapema Jumapili.