Kampuni ya Kenya Power imetoa wito kwa serikali kupiga marufuku biashara ya vyuma kuu kuu vya copper.
Hayo yamejiri baada ya afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Joseph Siror, kubaini kwamba kati ya mwezi Septemba mwaka 2023 na mwezi Agosti mwaka wa 2024, kampuni hiyo ilipoteza transfoma 110 za thamani ya shilingi milioni 137 kupitia wizi wa mitamb hiyo.
Siror alisema ni busara kwa wafanyabiashara wa vyuma kuukuu kubaini wanaowauzia vyuma hivyo hasa copper na Alluminium walikotoa vyuma hivyo ili kusaidia kubaini vinakotoka na kukablii wizi wa mitambo hiyo.
Siror aliongeza kwamba wizi wa mitambo ya transfoma umeathiri bishara na utoaji huduma muhimu kote nchini na kusababisha hasara kubwa miongoni mwa wateja wa umeme.
Aidha Siror alipongeza sheria ya bunge ya mwaka 2019 kuhusu nishati ambayo imeharamisha mtu yeyote kuhitilafiana na vyombo vya umeme bila idhini, wizi wa mitambo ya stima au uharibifu wa taa za barabarani.
Sheria hiyo inatoa faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha miaka 5 gerezani au vyote viwili kwa yeyote atakayepatikana na hatia.