Rais Ruto awatuza Migori Youth FC basi jipya

Migori Youth walitwaa ubingwa wa Ligi ya NSL,kwa kuzoa alama 81 baada ya kushinda  mechi 25,kwenda sare 6 na kupoteza saba katika msimu uliokamilika maajuzi.

Dismas Otuke
2 Min Read

Rais William Ruto ameikabidhi klabu ya Migori Youth FC, basi jipya baada ya kushinda taji ya ligi kuu daraja ya kwanza (NSL),na kupandishwa ngazi kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Hafla hiyo imeandaliwa siku ya Jumatatu katika Ikulu ya Nairobi, na kuhudhuriwa na maafisa klabu hiyo pamoja na viongozi wa kaunti ya Migori.

Akizungumza baada ya kukutana na wachezaji wa Migori, Rais alikariri azma ya serikali yake kuboresha miundombinu ya michezo nchini ikiwemo kaunti ya Migori ili kuchochea ukuzaji vipaji.

Aliongeza kuwa basi hilo litawawezesha wachezaji wa timu hiyo kusafiri kwa mechi  za Ligi kuu na pia kusafiri kwa minaajili ya mazoezi.

Rais pia alitumia fursa hiyo kuipongeza timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 17,kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili jana.

Migori Youth walitwaa ubingwa wa Ligi ya NSL,kwa kuzoa alama 81, baada ya kushinda  mechi 25,kwenda sare 6, na kupoteza saba katika msimu uliokamilika maajuzi.
Wakati uo huo Rais Ruto mapema Jumanne anatarajiwa kuikaribisha timu ya Kenya ya wanawawake(Harambee Starlets ) katika Ikulu .
Timu hiyo ilifuzu kushiriki fainali za Kombe mataifaifa ya Afrika WAFCON kwa mara ya pili mwaka huu.
Kipute cha WAFCON kitaandaliwa nchini Morocco kuanzia Julai 26  hadi Agosti 16.
Share This Article