Uswizi ilikuwa timu ya mwisho kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuwabandua Colombia kwa matuta ya penalti 4-3 kufuatia sare tasa katika dakika 120 za mchuano wa awamu ya 32 uliosakatwa mjini Vancouver, Canada Jumanne usiku.
Uswizi ambao wamerejea katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1954, watakumbana na mabingwa watetezi Argentina katika kwota fainali.
Argentina walihaha kabla ya kuwashinda Misri mabao 3-2 na kujikatia tiketi kwa robo fainali.
Kwota fainali zitaanza Alhamisi, Julai 9 huku Morocco wakipambana na Ufaransa kisha Ijumaa, Julai 10, Uhispania itoane kijasho na Ubelgiji.
Uingereza watakuwa ugani Miami dhidi ya Norway Jumamosi, usiku wa manane nao Uswizi wahitimishe ratiba dhidi ya Argentina mapema Jumapili.