Kenya imeimarisha hatua za kukabiliana na Ebola, asema Kindiki

Martin Mwanje
1 Min Read

Kenya imeimarisha hatua za kukabiliana na Ebola kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC. 

Hatua hizo ni pamoja na kuimarisha uangalizi katika maeneo ya kuingia nchini.

“Hatua za Kutosheleza za Udhibiti wa Maambukizi (IPC), uangalizi wa mipakani na maeneo mengine ya kuingia nchini, kuwakusanya wahudumu wa afya na bidhaa tiba pamoja na uanzishaji wa vituo 23 vya kuwatenga na kuwatibu wagonjwa unaendelea,” alisema Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki kwenye taarifa.

“Kwa sababu ya uunganikaji wa hatua za ueneaji na udhibiti, Kenya inafanya kazi na washirika wa kimataifa na kikanda ili kuhakikisha hatua zote muhimu za binadamu, kifedha na zingine ili kuangazia suala hilo.”

Prof. Kindiki aliyasema hayo alipokutana na Waziri wa Afya Aden Duale, na Makatibu Mary Muthoni na Dkt. Ouma Oluga na maafisa wengine wa wizara waliomtaarifu hatua walizoweka ili kujiandaa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

Share This Article