Monica Juma awasili Vienna kuanza rasmi majukumu yake

Tom Mathinji
2 Min Read
Monica Juma awasili Vienna, kuanza majuku yake kama Mkurugenzi Mkuu wa afisi za UN.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa afisi za Umoja wa Mataifa Jijini Vienna ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa afisi za UN kuhusu mihadarati na uhalifu (UNODC) Monica Juma, amewasili Jijini Vienna tayari kuchukua wadhifa wake mpya.

Alipowasili kwenye afisi hizo, Juma alisema atatumia tajiriba yake katika maswala ya ulinzi, usalama na diplomasia katika juhudi za Umoja wa Mataifa (UN), kukabiliana na changamoto zinazoshuhudiwa za ukosefu wa amani na usalama.

Aidha, alisema atajizatiti kukabiliana na mihadarati, uhalifu wa kupangwa, ufisadi na ugaidi ili kuhakikisha ulimwengu ulio salama na unaozingatia haki.

” Nina furaha kuanza awamu yangu katika afisi za Mkurugenzi Mkuu wa afisi za UN Jijini Vienna,” alisema Juma.

Kabla ya kuteuliewa kwake kwenye wadhifa huo, Juma alihudumu wadhifa wa Mshauri Mkuu katika afisi ya Rais na katibu katika Baraza la Usalama nchini Kenya.

Awali alihudumu kama Waziri wa Nishati, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Nje. Pia alihudumu kama kaimu Waziri wa Petroli na Madini.

Monica Juma alihudumu kama balozi wa Kenya nchini Ethiopia na Djibouti, mawakilishi wa kidumu wa Kenya kwenye Umoja wa Afrika, Shirika la Maendeleo la IGAD na katika Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika.

Juma aliteuliwa kwenye wadhifa huo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mnamo Machi 6 ,2026.

Share This Article