Idadi ya walioambukizwa Ebola yafika 3,500 DRC

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 3,500 waambukizwa Ebola nchini DRC.

Zaidi ya watu 3,500 wameambukizwa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). 

Wizara ya Mawasiliao na Vyombo vya Habari imesema aina hiyo ya Ebola ndiyo inayoenea zaidi katika historia ya taifa hilo.

“Aina hii ya Ebola ndio inayoenea zaidi tumewahi shuhudia,” aliema Kaimu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Chakula  Carl Skau.

Kulingana na Skau, ulimwemgu unapaswa kuwa makini sana kuhusu kuenea kwa ugonjwa huu.

Hadi kufikia sasa watu 1,556 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, huku kiwango cha maafa kutokana na Ebola kikifika asilimia 44.1, kulingana na data kutoka Wizara ya Afya ya Umma.

Wagonjwa 807 wametengwa au wamelazwa hospitalini, wengine  626 wakiripotiwa kupona ugonjwa huo.

TAGGED:
Share This Article