Wakazi wa Mandera waandamana kulaani mauaji ya watu sita

Tom Mathinji
1 Min Read

Wakazi wa Mandera wameandaa maandano kulaani mauaji ya watu sita kwenye shambulizi lililotekelezwa katika barabara ya Arabia–Mandera.

Waandamanaji hao walipita katika mji wa Mandera wakitoa wito kwa asasi za usalama kuchukua hatua za haraka dhidi ya waliohusika.

Aidha, wakazi hao walitaka vikosi kutoka Jubaland vinavyohudumu katika eneo la Omar Jillow kuondoka mara moja, huku wakihusisha shambulizi hilo na vikosi hivyo.

Wakiwa wamebeba mabango, waandamanaji hao walielekea hadi kwa afisi za Kamishna wa Kaunti kuwasilisha malalamishi yao.

Kulingana na wakazi hao, wale waliohusika na shambulizi hilo walitoka katika eneo la Omar Jillow,  wakitaka mwingilio wa kiusalama katika eneo hilo.

Akiwahutubia wakazi hao, Kamishna wa Kaunti ya Mandera James Chacha, aliwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa watulivu na kutoa fursa kwa asasi za kiusalama kushughulikia swala hilo kwa utaalam.

TAGGED:
Share This Article