Rais William Ruto amesema Kenya itashirikiana na Norway katika sekta ya uchumi wa baharini ili kuhakikisha Kenya inanufaika kikamilifu kutokana na rasilimali ya majini.
Ruto amesema hayo leo Jumanne alipokutana na wadau wa sekta ya majini mjini Oslo, wakiwemo viongozi wa chama cha wamiliki wa meli nchini Norway.
Alisema kuwa Kenya itashirikiana na Norway katika bandari za Lamu na Mombasa, hatua itakayopanua uwezo wa Kenya wa kujenga meli.
Rais pia alipongeza tangazo la kampuni ya meli ya Wilhelmsen Ship Management na kampuni zingine za Norway, zilizoahidi kuwaajiri Mabaharia 1,000 kutoka Kenya ifikiapo mwaka 2030, wakiwemo 120 ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu.