Serikali kuwafidia watakaoathiriwa na ujenzi wa reli ya kisasa

Reli hiyo ya kisasa itakuwa na urefu wa kilomita 98 katika kaunti ya Narok, ikipita pia katika kaunti za Bomet, Nyamira, Kericho, Homa Bay, na Kisumu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali kuwalipa fidia wamiliki ardhi watakaoathiriwa na ujenzi wa reli ya kisasa SGR.

Serikali imetenga shilingi bilioni 25, kuwafidia wale wataoathiriwa na ujenzi wa reli ya kisasa ya Narok-Bomet-Kisumu ambayo ni sehemu ya mradi wa reli ya kisasa ya Naivasha-Kisumu- Malaba.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini, Philip Mainga, alisema Tume ya Taifa ya Ardhi inatekeleza zoezi la mazungumzo na umma kabla ya kulipwa fidia kwa wamiliki ardhi walioathiriwa na ujenzi huo.

Wamiliki ardhi hao wameelezea nia  yao kushirikiana na serikali kuhakikisha mazungumzo ya kulipa fidia yanafaulu.

Akizngumza kwenye mkutano huo wa mashauriano na umma, Mzee Stephen Ruto mkazi wa kijiji cha Kapkesosio, alisema jamii imekaribisha mradi huo, akiseme utaunganisha kaunti ya Bomet na kaunti zingine, pamoja na kanda ya Afrika Mashariki.

Reli hiyo ya kisasa itakuwa na urefu wa kilomita 98 katika kaunti ya Narok, ikipita pia katika kaunti za Bomet, Nyamira, Kericho, Homa Bay, na Kisumu.

Reli hiyo inalenga kuimarisha uchukuzi wa bidhaa zilizokuzwa hapa nchini ikiwa ni pamoja na Majani Chai, Kahawa na Sukari, hadi katika bandari ya Mombasa ili kuuzwa nje ya nchi.

Mradi huo pia unatarajiwa kubuni nafasi za ajira na kupiga jeki biashara ndogo ndogo.

TAGGED:
Share This Article