Ligi Kuu Kenya kuanza Jumamosi baada ya vuta ni kuvute

Mechi mbili zitapigwa Jumamosi Mathare United ikiwaalika APS Bomet uwanjani Police Sacco, kuanzia saa nane kabla ya Shabana kuwazuru Posta Rangers saa kumi n robo katika uchanjaa wa Wang'uru.

Dismas Otuke
1 Min Read

Msimu mpya wa Ligi Kuu Kenya mwaka 2026/2027 hatimaye utaanza Jumamosi Oktoba 10, baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na mizozo.

Mechi mbili zitapigwa Jumamosi Mathare United ikiwaalika APS Bomet uwanjani Police Sacco, kuanzia saa nane kabla ya Shabana kuwazuru Posta Rangers saa kumi na robo katika uchanjaa wa Wang’uru.

Michuano minne itasakatwa Jumapili Ulinzi Stars wakifungua ratiba na Tusker FC uwanjani Ulinzi Complex wakati 3K FC, waliopandishwa ngazi  wakiwa nyumbani uwanjani Moi katika kaunti ya Embu dhidi ya Mara Sugar.

Mabingwa wa Ligi ya NSL Migori Youth watawaalika  Police FC  uwanjani Awendo Green.

Nairobi United watakamilisha ratiba ya Jumapili dhidi ya Kenya Commercial Bank.

Mombasa United watachuana na Kakamega Homeboyz  Jumanne ijayo katika uwanja wa Mbaraki  kisha Gor Mahia wamalize udhia  dhidi ya Muranga Seal.

AFC Leopards watafunga ratiba ya raundi ya kwanza dhidi ya Bandari FC uwanjani Nyayo Jumatano ijayo.

Share This Article