Rais Trump kuhudhuria fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Uhispania

Jumla ya mechi 102 zimesakatwa tangu kuanza kwa patashika hiyo inayoandaliwa kwa pamoja na Mexico, Canada na Marekani na mabao 297 kufungwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuhudhuria fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Uhispania Jumapili hii katika uwanja wa New York, New Jersey mjini New York.

Trump hajahudhuria mechi yoyote uwanjani kwenye fainali za mwaka huu licha ya timu yake kucheza raundi ya 16.

Marekani ilijukumishwa kuandaa kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia mwaka huu mnamo mwaka wa 2018 katika  muhula wa kwanza wa Rais Trump baada ya kuishinda Morocco.

Fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia ambazo ni za 23 zilishuhudia timu 48 zikishiriki kwa mara ya kwanza ikiwa ongezeko kutoka kwa 32 za awali.

Jumla ya mechi 102 zimesakatwa tangu kuanza kwa patashika hiyo inayoandaliwa kwa pamoja na Mexico, Canada na Marekani na mabao 297 kufungwa.

Mashabiki milioni 6.65 wamehudhuria mechi 102 za fainali hizo ikiwa wastani wa mashabiki 65,351 kila mchuano.

Kyllian Mbappe wa Ufaransa na Lionel Messi wa Argentina wangali unyo kwa unyo katika ufungaji mabao, wakibusu nyavu mara 8 kila mmoja.

Share This Article