Waziri wa mawasiliano nchini Burundi Gabby Bugaga ameaga dunia kutokana na kile kilichotajwa kuwa alihusika kwenye ajali ya barabarani.
Rais wa Burundi Evereste Ndayishimiye alisema Alhamisi jioni kuwa Waziri huyo alifariki katika ajali.
Yamkini mwili wa marehe,ulipatikana na wakulima ukiwa ndani ya gari lake katika barabara isiyotumiwa sana eneo la Kivoga ,kilomita 10 kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura.
Bugaga ambaye pia ni Mwanahabari aliteuliwa waziri mwaka uliopita.
Kifo chake kimeibua maswali mengi baada ya kichwa chake kuwa na alama kubwa ya kukatwa ingawa gari lake halikuwa na dalili zozote za kuharibika kutokana na ajali inayosemekana kusababisha kifo chake.