Mgomo wa wahudumu wa daladala umeingia siku ya pili leo katika eneo la Tanga nchini Tanzania huku usafiri wa umma ukiathirika pakubwa.
Mgomo huo ulianza Aprili huku zaidi ya daladala 400, zikisitisha huduma na kuwaacha wasafiri kwenye njia panda.
Wahudumu wa daladala wanatetea kuhusu kuongezwa kwa bei ya mafuta hali ambayo imechangia kupungua kwa pato lao la kila siku.
Wenye dalaladala wanasema gharama ya uendeshaji biashara hiyo imekuwa juu kiasi kwamba ni vigumu kuafikia malengo ya pesa wanazohitajika kuwalipa wamiliki wa magari hayo ya biashara.