Nitafanya kila kitu kuwalinda Wakenya dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta asema, Ruto

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais William Ruto ameapa kuafanya kila liwezekanalo ili kuwalinda Wakenya kutoka na kupanda kwa gharama ya maisha ambayo inasababishwa na misukosuko inayoshuhudiwa Mashariki ya Kati.
Rais amesema haya mapema Ijumaa aliposaini kuwa sheria muswada  wa kupunguza ushuru wa thamani ya bidhaa VAT kutoka asilimia 16 hadi 8 kwa bidhaa zote za mafuta nchini.
Sheria  hiyo mpya ambayo itaanza kutekelezwa kwa  siku 90 wameongeza kipengee kinachoruhusu kuendelea kutumika kwa zaidi ya kipindi hicho endapo hali bado haitaiomarika  Mashariki ya Kati.
Muswada huo ulipitishwa na bunge la kitaifa ndani ya siku moja .
Bei ya mafuta ilipanda  kwa kati ya shilingi 10 na 9 kwa mafuta ya petroli na dizeli,mapema wiki hii siku moja baada ya bei hiyo kuongezwa kwa hadi shilingi 40 kwa lita moja.
Share This Article