Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC imewakamata washukiwa 9 kutoka Wizara ya Fedha kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ulaghai wa shilingi bilioni 1.57.
Washukiwa hao waliokamatwa kuhusiana wanazuiliwa katika makao makuu ya tume hiyo jijini Nairobi.
EACC inapanga kuwafikisha mahakamani kesho Jumatano, Agosti 19.