Magavana waunga mkono mjadala wa kitaifa

Mwenyekiti wa baraza la magavana Ahmed Abdullahi alisema kuwa magavana wataunga mkono mchakato huo.

Marion Bosire
1 Min Read
Ahmed Abdullahi - Mwenyekiti wa Baraza la Magavana

Baraza la magavana nchini, COG, limeunga mkono mjadala wa kitaifa huku magavana wakitoa wito wa ruwaza ya kudumu ya maendeleo inayohakikisha ukuaji sawa katika kaunti zote na inayolindwa dhidi ya mwingilio wa kisiasa.

Akizungumza katika kikao cha kuzindua mjadala huo wa kitaifa katika jumba la KICC jana, mwenyekiti wa baraza la magavana Ahmed Abdullahi alisema kuwa magavana wataunga mkono mchakato huo na kuhakikisha kwamba kaunti zinahusika kikamilifu katika kukusanya maoni kutoka kwa wananchi na sekta mbalimbali.

Abdullahi hata hivyo alionya kuwa mipango bora huenda ikasambaratika bila uongozi bora na uongozi wa kisiasa akisiema kuwa uongozi bora nchini utaamua iwapo ruwaza ya kitaifa inayopendekezwa itatekelezwa kwa ufanisi.

Abdullahi alisema kuwa mchakato huo unajiri huku ruwza ya sasa yam waka 2030 ikikaribia kufikia kikomo akitoa wito wa mfumo mpya wa kuiongoza Kenya baada ya ruwaza ya mwaka 2030.

Share This Article