Wizara ya Afya inaongoza juhudi za kuimarisha usalama wa chakula kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa, zile za kaunti, sekta za kibinafsi, na washirika wa maendeleo.
Katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni, ametangaza kuwa serikali imewasilisha mswada wa sheria ya kudhibiti usalama wa chakula na lishe, 2023, ili kuimarisha uratibu wa usalama wa chakula.
Akizungumza kwenye mkutano na washikadau wa siku ya chakula duniani, Muthoni alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa sekta mbalimbali katika kusimamia masuala ya usalama wa chakula.
Aliangazia mada ya mwaka huu, “Usalama wa Chakula: Jiandae kwa Yasiyotarajiwa,” ambayo inasisitiza haja ya hatua madhubuti na za haraka ili kukabiliana na hali hii.