WHO: Ugonjwa wa Ebola ulizuka miezi kadhaa DRC kabla kugunduliwa

Visa vilivyothibitishwa vya Ebola nchini DRC, sasa vimefika 4,200, vikiwemo vifo 1,900 kulingana na serikali ya DRC.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 4,200 waambukizwa Ebola nchini DRC.

Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema ugonjwa wa Ebola ambao unaenea kwa haraka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ulizuka mwezi Februari, kabla ya kutangazwa rasmi katikati ya mwezi Mei.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Mohamed Janabi, alidokeza kuwa baadhi ya dalili za ugonjwa huo zilihusishwa kimakosa na magonjwa ya Malaria na Kipindupindu.

“Tunafuata virusi, virusi hivyo viko mbele yetu,” alisema mkurugenzi huyo.

Visa vilivyothibitishwa vya Ebola nchini DRC, sasa vimefika 4,200, vikiwemo vifo 1,900 kulingana na serikali ya DRC.

Aina hii ya Ebola ya Bundibugyo hadi sasa haijapata chanjo au matibabu.

Makundi ya Maafisa wa Afya  husafiri katika maeneo ya mashinani katika juhud za kukabiliana na ugonjwa huo, licha ya baadhi ya maeneo nchini humo yakikabiliwa na ukosefu wa maji hatua inayohatarisha zaidi maisha ya wakazi.

Aina ya Ebola ya Bundibugyo imetajwa kuuwa watu haraka ikilinganishwa na aina za Ebola ambazo zimewahi nakiliwa ikiwa ni pamoja na iliyozuka kati ya mwaka 2014-2016 Afrika Magharibi iliyosababisha vifo vya watu 11,000 kati ya visa 28,000 vilivyonakiliwa.

Share This Article