Washukiwa wanne wa mauaji ya Mbunge wa Kasipul, Chares Ong’ondo Were, waliokamatwa Jumapili, wamefikishwa mahakamani leo Jumatatu kujibu mashtaka .
Wanne hao wamehojiwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya JKIA.
Kulingana na polisi mshukiwa mkuu ambaye anadaiwa kumpiga risasi marehemu, alikiri kuwa afisa wa polisi ingawa hajakuwa akiripoti kazini.
Polisi siku ya Jumapili waliwakamata washukiwa hao wanne, gari na pikipiki waliyotumia kutekeleza uhalifu huo.
Marehemu Mbungo huyo anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo bunge la Kasipul Ijumaa hii, Mei 9.
Wakati huo, Mkuu wa Polisi, Johansen Oduor, alithibitisha kuwa Were, alifariki kutokana na kufyatuliwa risasi tano kifuani na kwenye bega na kuharibu vibaya viungo muhimu, hali iiyoondolea mbali uwezekano wa kupona.