Rwanda imeanza mazungmzo ya kuwapokea wahamiaji waliofurushwa kutoka nchini Marekani, na mataifa mengine ya magharibi kwa kuwa huko bila stakabadhi.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, amesema wako katika hatua za mwanzo kujadiliana na Marekani kuhusu kuwapa hifadhi wakimbizi watakaotimliwa .
Mji wa Kigali ulisaini makubaliano na Uingereza mwaka 2022, kuwapa hifadhi maelfu ya wakimbizi, kabla ya Waziri Mkuu wa Uingereza aliyechaguliwa Keir Starmer kubatilisha.
Rais Donald Trump wa Marekani, alianzisha sheria kali punde baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili wa kuwafurusha raia wote wa kigeni walio nchini humo bila stakabadhi.
Shirika la Umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi -UNHCR, limeonya kuwa huenda kukazuka mzozo wa kibinadamu kwa baadhi ya wakimbizi watakaopelekwa Rwanda, huenda wakarejeshwa tena katika mataifa waliyotoroka vita.