Wandayi: Wakenya watapata umeme wa gharama nafuu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa nishati Opiyo Wandayi.

Serikali inalenga kuimarisha mikakati yake ya kuhakikisha wakenya wanapata nguvu za umeme za kutegemewa, za kutosha na za bei nafuu, ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa hili.

Alipozuru kituo kidogo cha kusambaza umeme cha Juja, waziri wa nishati Opiyo Wandayi akiwa ameandamana na wakurugenzi wa bodi ya kampuni hiyo na wafanyakazi, walijadili kuhusu sera na ushirikiano na asasi zingine za serikali kutatua changamoto zilizopo.

 “Bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo, imenifahamisha kuhusu mpango wa kimkakati ya muda wa miaka mitano ijayo na hatua zilizopigwa hadi sasa,” alisema Wandayi.

Waziri huyo alisema kampuni hiyo inajizatiti kutosheleza mahitaji ya wateja wake kupitia uadilifu.

“Serikali imekariri kujitolea kwake kufanyia mabadiliko kampuni hiyo, ili ikumbatie teknolojia, inayotunza mazingira na inayotoa huduma kwa uadilifu,”  aliongeza waziri huyo.

Aidha waziri Wandayi alisema serikali itaendeleza msako dhidi ya uunganishaji haramu wa umeme, huku  akitoa wito kwa umma kuzingatia utaratibu uliopo wanapounganishiwa umeme.

Share This Article