Wakenya kwenye mtandao wa X walifurahia kionjo cha kibao kipya cha injili kilichoporomoshwa na msanii maarufu wa Tanzania Christina Shusho, kijulikanacho kama Zakayo.
Kionjo cha wimbo huo kilikuwa na zaidi ya wafuasi nusu milioni wengi wao kutoka Kenya kupitia mtandao wa X Jumatatu jioni .
Christina Shusho doing the Lord’s work from across the border. pic.twitter.com/0I6elLYCr3
— 𝐒𝐭✰𝐫𝐛𝐨𝐲 (@StarBuoy_) April 22, 2024
Kibao hicho kitakuwa cha punde zaidi kwa msanii huyo maarufu baada ya kuporomosha kibao cha Shusha nyavu ambacho kilipendwa zaidi husuan nchini Kenya.
Kibao hicho kipya cha Zakayo kinachotokana na hadithi kwenye bibilia kuhusu mtoza ushuru Zakayo aliyekataa kushuka kutoka juu ya mti wa Mukuy, licha ya kuamrishwa na yesu.
Zakayo alipanda juu ya mti akitaka kumwona Yesu alipokuwa akipita.