Sophie Gombya asimulia kuhusu tukio la kuogofya akiwa Rais UMA

Mwanamuziki wa kike alimjia afisini na begi iliyokuwa na mwili wa mwanawe akitaka nauli ya kurejea nyumbani.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uganda Sophie Gombya amesimulia kuhusu tukio la kuogofya alilokumbana nalo siku ambayo aliamua kujiuzulu kama Rais wa chama cha wanamuziki wa Uganda UMA.

Kulingana naye, alipokea simu kutoka kwa mwanamuziki huyo wa kike kutoka eneo la Iganga ambaye alikuwa anataka usaidizi wa UMA kuhusiana na matibabu ya mwanawe katika hospitali ya Mulago.

Siku tatu  baadaye, mwanamuziki huyo ambaye hakufichua jina lake alifika kwenye afisi yake akiwa na begi ambayo aliitupa kwenye meza yake akilalamika jinsi mwanawe alifariki.

Mwanamke huyo alifungua begi hiyo akamwonyesha Gombya mwili wa mtoto wake akitaka ampe fedha za kufadhili usafiri wake hadi Iganga kwa ajili ya mazishi ya mtoto huyo.

Sophie anasema baada ya kuona mwili huo alijawa hamaki na kumzomea mhusika.

Gombya alianza kazi rasmi kama Rais wa UMA mwezi Mei mwaka 2019 na kujiuzulu mwezi Julai mwaka 2020 baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja na mwezi mmoja pekee.

Katika barua yake ya kujiondoa hata hivyo hakutaja kisa hicho bali alielezea kwamba alikuwa anaingilia siasa na katika ya UMA hairuhusu kiongozi kushikilia uongozi na kuwa kwenye siasa.

Website |  + posts
Share This Article