UDA yaimarisha kampeni za kuwinda kura Ol Kalou

Uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Ol Kalou utaandaliwa Julai 16 kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo David Njuguna Kiaraho mapema mwaka huu. 

Martin Mwanje
2 Min Read
Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, akiwa na viongozi wengine wakimfanyia kampeni mgombea wa UDA awali

Viongozi wa chama tawala cha UDA wameendelea kukita kambi katika eneo bunge la Ol Kalou kwa nia ya kuwashawishi wakazi kuunga mkono mgombea wao Muchina Nyagah kwenye uchaguzi mdogo ujao. 

Nyaga atatoaja kijasho na mgombea wa chama cha DCP Sammy Ngotho chake Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua.

Viongozi hao walijumuisha Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Nyahururu Faith Gitau, wabunge Mwangi Kiunjuri wa Laikipia Mashariki na Anthony King’ara wa Kieni, mbunge mteule Sabina Chege na mbunge wa zamani wa Mathira George Gachagua miongoni mwa wengine.

Wote hao walihutubia mikutano ya kisiasa katika wadi mbalimbali katika eneo bunge hilo na kutoa wito kwa wakazi kumuunga mkono Nyagag ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya serikali katika eneo hilo.

Na huku upinzani ukiishutumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kutumia miradi ya maendeleo kama chambo ya kuwashawishi wapiga kura, viongozi hao walitetea utekelezaji wa miradi hiyo wakisema ilinuia kubadilisha maisha ya wakazi wakati ikiongeza kasi ya ukuaji uchumi.

Uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Ol Kalou utaandaliwa Julai 16 kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo David Njuguna Kiaraho wakati akitibiwa katika hospitali moja jijini Nairobi.

Uchaguzi huo unachukuliwa kama mizani ya kupimana ubabe wa kisiasa kati ya Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki na mtangulizi wake Rigathi Gachagua katika eneo la Mlima Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Share This Article